IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE
JINSI YA KUSHINDA TAMAA ZA MWILI (PART 1)
Na :Shujaa Charles Mwaisemba
Moja ya mambo ya Msingi sana katika Kizazi cha leo hasa kwa Vijana wengi hata yamkini waliokoka wako katika kipindi kigumu sana na kizito cha Kulemewa na TAMAA ZA MWILI . Tumesikia taarifa nyingi za Watu ambao haujawadhania waliokuwa moto sana na wanampenda Mungu lakini nao Kwa kutokuyajua haya wamejikuta wakianguka katika dhambi za Tamaa za mwili , Wengi wameanguka katika Uasherati na wengine wengi pamoja wanaweza wakajizuia kufanya uasherati au kulala na mdada au mkaka, lakini leo wamechukuliwa na Kupiga Punyeto/Mastrubation na kujimalizia tamaa wao wenyewe na Wengine wamefika Mbali sana Hata kuwakiana tamaa wenyewe kwa wenyewe yaani Watu wa jinsia Moja kwa ulawiti na hata wengine Ushoga na Usagaji
Moja kati ya mambo yanayowasumbua hawa watu wanaofanya hivyo ni kwamba kwa sasa wanatamani kuacha au kutoka katika hali hizo lakini kila jitihada zao zote wanajikuta wanakaa muda mfupi lakini wanarudia kule kule. Wanatubu na kutubu lakini hawaoni tena uwezo wa kushinda hizo dhambi mpaka wengi wao mpaka sasa wapo wanaishi wameshakata tamaa na wameyafanya hayo maisha kama ni sehemu ya maisha yao na bado wanakuja kanisa na wanafanya huduma mbalimbali lakini Wameshaizoelea dhambi hizo.
Maandiko yanasema Tusimpe ibilisi EFESO 4:27.Lakini watu hawa walimpa Ibilisi nafasi katika maeneo ambayo tutayaona hapo mbele kwenye somo hilo.Lakini zaidi sana Wengi wanafanya wanayofanya ya Uchafu kwasababu wengi wanafanya wakijua au wakidhani kwamba watatubu tu na kuirudia ile hali yao ya mwanzo waliyokuwa nayo.Lakini cha Ajabu tangu waingie huko wamejikuta hawawezi kuninasua wala kujisaidia waachane na tabia hizo na mbaya zaidi wanaficha ficha dhambi zao wala hawataki kueleza ili wapewe msaada matokeo yake kila siku wanapelekwa mbali zaidi.
Ni makusudi ya Somo hili Kuangali Baadhi ya Maeneo ambayo ndio shetani anatayatumia kwa kujua au kutokujua kuchochea Tamaa za mwili kwetu ambazo ndizo zinachochea Kwenda kufanya Ucahafu wa namna hiyo kama tulivyoona. Na Shetani hasa hizi nyakati za mwisho akijua Muda wake umeisha ndio amemwaga roho 3 za Uchafu ambazo zimeuvaa ulimwengi wote hasa vijana na hatataka kuwapoteza hata Yamkini walio wateule UFUNUO 16:13
{EFESO 2:3}
ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu , tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia , tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Katika tamaa za miili yetu yanatokana na mambo mawili makuu
Mapenzi ya nia zetu
Mapenzi ya Mwili
TAMAA ZA MWILI ZITOKANAZO NA MAPENZI YA NIA ZETU
Haya mapenzi ya Nia zetu yanatokana na jinsi ambayo tunachukuliwa na namna au mambo ya kidunia ambayo yanafanywa katika Ulimwengu ambayo ndiyo yanapelekea na sisi kuvutwa na kutaka kufanya kwa namna yao au kuenenda kama wao.Mapendi ya nia zetu yanapoharibiwa na mambo ya kidunia yanayotuzunguka ndio yanapelekea kuamsha Tamaa za Miili yetu na kujikuta tunafanya dhambi na kumkosea Mungu
Hivyo ukiwa unapenda mambo ya kidunia au unataka kufanya kila kitu kama mataifa wanavyofanya lazima utavutwa na tamaa za mapenzi ya nia Zetu.Unapoangalia mataifa wanavaa mavazi yanabana miili yao au Yanachora miili yao, au yanaonyesha baadhi ya viungo vya miili yao nawe unapenda unaona kama wao wanapendeza na unaaanza kuvaa kama wao au kutaka kutokeleza kama wao kumbe hujui wao walifaa yale wanayoyavaa au walifanya yale wanayoyafanya kwa kufuatisha nia zao mbaya kwa kufuata namna ya Dunia
Mambo ya kidunia au namna ya ya dunia yapo mambo mengi sio mavazi tu bali katika maeneo mengi.Cha msingi tuwe makini tusifanye kama wao wanavyofanya bila kujua kuna nini nyuma ya nia zao.
Hivyo tuwe makini sana na kuchukiliwa namna za dunia na mambo wanayofanya mataifa na sisi tukataka kuyafanya, maana wao wanafanya katika ubatili wa nia zao.Tukiwa mbali na mambo hayo yote ndio tutakuwa mbali na Tamaa za mwili zitokanazo na Mapenzi ya nia Zetu
{WARUMI12:2}
_[2]And be not conformed to this world: but be ye transformed by the renewing of your mind , that ye may prove what is that good, and acceptable, and perfect, will of God._
_Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu , mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu._
{WAEFESO 4:23-24}
_na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu ;mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli._
Sasa ili kutoka kwenye tamaa hizi zitokanazo na nia zetu ni mpaka tugeuzwe upya nia zetu kwa Neno la Mungu na Roho mtakatifu. Ikiwa na maana ni lazima tujifunze Neno la Mungu kwa wingi na likae ndani yetu ndio hatutaweza kuchukuliwa na hizo za dunia au roho za kufuatisha namna ya dunia na mitindo yake.Lazima tuwe tayari kukaa mahali ambapo mambo ya kidunia yote yanakemewa kwa nguvu kubwa vinginevyo tutajikuta hatuna tofauti ya maisha yetu kabla ya kuokoka na baada ya kuokoka
Tukikaa mahali ambapo Mchungaji anaona ni sawa wanawake kuvaaa vyovyote au kufanya mambo yoyote ya kidunia katika mitindo yake hiyo itatufanya Kuvutwa tu na hizi tamaa za mwili maana ndizo zinachochewa kwa nguvu na tunaweza tukawa tunajiita tumeokolewa lakini tusiione mbingu kwasababu ya mambo ya kidunia tunayoyafuatisha
TAMAA ZITOKANAZO NA MAPENZI YA MWILI
Mungu katika uumbaji wake ndiye aliyetuwekea tamaa hii ya miili yetu wala haitoki kwa shetani ambayo hiyo inapaswa kulindwa na kutokuendeshwa nayo kwa kufuata mapenzi ya mwili yanavyotaka au kwa kutoruhusa vitu vinavyohamsha tamaa hizo
{MWANZO3:16}
_Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo , naye atakutawala._
Tamaa hii ipo tu ndani yetu ,Ni kama gari lenye mafuta tayari yaani ukiliwasha tu lazima liwake na liende ila ukiliacha litakaa hivyo hivyo.
Kuna mambo katika mwili ni ya kawaida kuwa hivyo sio dhambi yakiwepo hivyo maana ni asili ya miili yetu ndio ipo hivyo.Ni kama usipooga lazima utanuka tu hata kama umejawa neno na hata kama unanena kwa lugha
{WIMBO ULIO BORA3:5}
_Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe. Bwana Arusi na Kundi lake Wakaribia_
Mapenzi haya ya mwili yanakuwa stimuleted pale tu tunapoyachochea na kuyaamsha ndipo yanafanya kazi kwa kutimiza matakwa ya mwili.
Kama umeyachochea mwenyewe na kuyaamsha mwenyewe hapo hata kama ukiomba kwa kunena kwa lugha au hata kama umejawa Neno kiasi gani lazima ukajinyooshe(lazima akatimize mapenzi yake) maana mapenzi ya Mwili yamezidiwa na mapenzi ya Roho hivyo lazima tu ufanye yale yanayotaka mwili hata kama umejazwa Roho kwasababu tu umeyachochea na kuaamsha
{WAGALATIA 5:16-17}
_Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili .Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili ; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka._
Umeona maanake kwa msingi huo ikiwa wewe ndio umetengeneza mazingira ya kuuamsha na kuuchochea mwili wako katika mapenzi ya mwili hapo Roho lazima itashindwa na mwili na lazima utafanya mapenzi ya mwili utake usitake
Ndio katika kipindi hiki unakuta watu wanashangaa au wewe unajishangaa kweli mpaka nimejikuta nimefanya uchafu huu au ule? Wakati unajijua Roho mtakatifu unaye na Neno unalo lakini lazima utazidiwa na mwili kwasababu umeyaamsha mapenzi na kuyachochea.Sasa maandiko yanasema Tusiyachoche Mapenzi haya
Muda wangu hautoshi kuelezea mambo yote kwa undani juu ya hili , ila niseme hapa ndipo wengi uanguka dhambini na kwa kufanya uasherati au uzinzi au tamaa nyingine za uchafu kwasababu ya mambo waliyoyatengeneza wenyewe yaliyopelekea Kuanguka katika tamaa hizo za mwili zinazotokana na mwili
Ningekuwanna muda wa kutosha ningeleeza kwa urefu au kwa undani juu ya baadhi ya mambo ambayo ndio vichochea vikubwa ya Tamaa ya miili yetu kuwaka hata kufuata mapenzi ya mwili na kufanya uchafu na machukizo ya kutisha ila hapa kwa leo nitakwenda kutaja baadhi ya maeneo ya msingi tu kwa uchache ambayo ndiyo vuchocheo vikubwa sana vinavyofanya wengi kuanguka katika tamaa za mwili na uasherati na uzinzi
1) Kuwepo na Uhusiano Mkubwa kati ya mdada na mkaka(Uhusiano wa mwanaume na mwanamke)
Hili swala ni chanzo kikubwa sana cha kuamsha Tamaa za miili yetu hata kujikuta tunafuata mapenzi ya mwili na hatimaye ndiyo iliyopelekea leo watu wengi waliokoka wanajikwaa na kuanguka dhambini katika uchafu wa namna ya kutisha na mpendwa mwenzake
Hili ni hasa pale kaka au dada anapojifanya yupo rohoni sana na kujifanya hana hisia za mapenzi na dada fulani bali wapo nae karibu tu kama rafiki yake mwingine wa jinsi yake.Hili ni kosa kubwa sana ingawa kizazi hiki cha uchafu na uzinzi hakipendi kuambiwa habari hizi. Na sina maana hatuwezi kuongea au kuwasiliana na wadada bali ninachokizungumza hapa ni Ukaribu au Mawasiliano ya karibu hata kama sio ya uchafu au sio mabaya!!!
Hilo swala kijiamini kulikopitiliza ndiko kulikomfanya Daudi ajinyooshe(Afanye uzinzi) kwa mke wa huria maana alijiona wa rohoni sana kiasi cha kwamba hawezi kuangushwa kwenye uzinzi akaruhusu tu macho yake kuona uchi wa mwanamke.Hata Samson akajifanya kiroho akalala mapajani pa Delila, unategemea nini kitatokea kama sio Uasherati!!!
Hata ukiwa rohoni vipi na umejaa neno vipi, ukiruhusu Ukaribu wa dada na kaka kama ulio nao kwa mtu wa jinsia yako, ujue lazima tu siku moja utajinyoosha(Mtafanya uzinzi /uasherati).Unaweza ukajisifu kuwa wewe unajitambua na huyo dada au kaka unamchukulia kama kaka yako au dada yako lakini nakwambia ipo siku mtajinyoosha,Ninyi endeleeni nawapa mda tu
Mwanamke na mwanaume ni kama Unlike charges lazima tu zita attract each other . Lazima tu utakuwa na hisia za mwili, kama sio wewe basi mwenzio ndiye anakuwa nazo ambapo wewe hujui na ipo siku Shetani akiwapeleka sehemu nzuri lazima mtajinyoosha tu
Hivyo ukaribu wowote lazima utawaingiza dhambini yaani lazima utaamsha tamaa za mwili na Mwili ukishazidiwa na tamaa hizo lazima utajinyoosha tu.
Hivyo jitahidi kutokuwa na ukaribu na kaka fulani au dada fulani kiasi kwamba mpaka watu wanawahisi Uasherati juu yenu na hata kama kweli katika ukaribu wenu hamjawai kutamaniana au kufanya lolote la kimwili ,ujue ikiwa mkiwa na ukaribu unaotia mashaka wa wa kupitiliza Ujue Unafanya Dhambi ile ile ya Uasherati
{WAEFESO 5:3}
Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe , wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
Maandiko hayasemi msifanye uasherati tu bali UASHERATI USITAJWE KWENU KAMWE . Kumbe kitendo cha Uasherati kutajwa kwetu kwa uhusiano wetu na kaka fulani au dada fulani tunahesabika wote ni waasherati hata kama mjawai kukutana kimwili.
Hivyo usijitete mbona hamjawai kukutana kimwili na kaka fulani au dada fulani bali pale unapotengeneza mazingira ya kuhisi uasherati kwenu kwa ukaribu wenu ujue Unahesabika mkosaji maana mandiko yanasema tuwe na dhamiri isiyo na hatia si Tu mbele za Mungu bali hata mbele za wanadamu.Sasa ninyi sio kwamba ni wachumba au mme na mke lakini kila mahali tunawaona mpo pamoja, kwa kaka upo na kwa dada upo!! Hivi unafikiri tukiwaita waasherati tunakosea au tumewawazia vibaya eti kwasababu hamjafanya uasherati?
Hata kama ni Mchumba wako bado haikupi kibali cha kuanza hadi kutembeleana vyumbani mwetu na kupikia na kulala pamoja kama mume na mke.Bado tukiwa katika uchumba kutakuwa na mipaka fulani ambayo haitawaingiza kufanya uasherati kabala ya ndoa.Lakini cha ajabu ndoa nyingi za hao wanaojiita wameokoka zinakuwa zimeanzia kwenye uchumba ambao tayari wameshaanguka dhambini na kufanya uasherati kwa madai eti ni mchumba wako!wanadai wanaonjeshana ili kumpima kwamba ni mzima au la! kufanya hivyo ni uhuni na haipaswi kuwa hivyo kwetu tuliokoka
Hivyo hoja yangu hapa ni kwamba ukaribu wa dada na kaka unachochea sana tamaa za miili yetu hata kufuata mapenzi ya mwili.Lazima mmoja au wote mkapendana na lazima Siku mtajikuta kwenye uasherati, nawapo siku tu
Usikose kufuatilia Sehemu ya pili ambapo tutaendelea kuona maeneo ya muhimu yanayohusika kuchochea Tamaa za mwili .

0 Comments