Sehemu ya 2 JINSI YA KUSHINDA TAMAA ZA MWILI

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

JINSI YA KUSHINDA TAMAA ZA MWILI (Sehemu ya Pili)

Shujaa Charles Richard Mwaisemba

TAMAAA ZITOKANAZO NA MAPENZI YA MWILI

Tunaendelea kutoka tulipoishia ambapo tupo kwenye kuangalia maeneo ambayo ndiyo tukimpa ibilisi Nafasi kwayo yanachochea kuamsha Mapenzi ya Mwili ambayo yalikuwa yametulia.Tulishaona eneo la kwanza lipo kwenye mahusiano kati ya dada na kaka na sasa tunaendelea na sehemu ya Pili

2) Yale mambo tunayoyaona au kupenda kuyaangalia mara kwa mara iwe ni movie au Tamthilia au Maigizo ambayo yanayoamsha Tamaa za kimapenzi

{2 SAMWELI 11:2}
Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.

Unaona Tatizo lilimkuta Daudi si kwamba hakuwa na Neno au hakuwa amejazwa Roho ila aliangalia video yaani akaruhusu macho yake akamuona Mwanamke anaoga nae aliporuhusu tu kuendelea kuangalia ndipo akanasa na kuanguka kwenye Tamaa za mwili zitikanazo na mapenzi ya Mwii

Hapa napo ndio mtego mkubwa sana wa Ibilisi na wengi wanaangukia hapa pia.Wanaweza wakawa wapo vizuri kwenye maombi au Neno lakin pale wanaporuhusu macho yao kuangalia mambo maovu au video au picha ambazo zinanajisi roho zao hivyo kuchochea tamaa za mwili kuwepo juu kuliko matakwa ya roho

Yapo maigizo au Tamthilia au Movie ambazo wengi wetu tunapenda kuziangalia ambazo shetani kwa makusudi kabisa Shetani anaachilia ziwepo na mapenzi mapenzi au uchafu chafu fulani ambao ukiruhusu tu macho yako kupenda kuziangalia angalia basi unavamiwa na unayaamsha mapenzi hayo ya mwili

Shetani ni mjanja sana hawezi kuleta movie nzima kuwa ni ya uchafu bali atachanganya na vitu baadhi vya kujifunza na kukuburudisha lakini ndani yake ndio atakuwa anapenyeza hivyo vitu ambavyo vinachochea na kuamsha hisia za mwili na leo amefanikiwa kuingia hadi kwenye hiki kitu tunachokiita Christian movie

Nimeshuhudia vijana wengi ambao mara baada ya kuangalia movie hizo ndio wanakuwa na hisia kali hata kutafuta wanawake au wakikosa ndio wanaingia kupiga punyeto au masturbation,Najua wengi humu wananielewa sana

Kuna wakaka humu na kwinginepo mpaka sasa ni kweli anaogopa kutembea na dada fulani lakini wanateswa na hili swala la punyeto na anatamani kuacha ila anashindwa na anaogopa kuwaeleza watu maana anaona ni jambo la aibu au unaweza kumuona hajaokoka

Nisikilize ishu sio kwamba hujaokoka inawezekana umeokoka ila wewe ndio uliruhusu kuangalia mapicha au mavideo hayo ambayo kidogo kidogo ndio yakakuhamisha mpaka uko hivyo ulivyo, na unatamani kuacha huwezi, kila ukiacha unakaa wiki tu unarudia kulekule

Wewe endelea kuficha dhambi zako , hivyo hautasaidika bali ndio unazidi kupotezwa na kupelekwa mbali zaidi.Hivyo ni heri utafute msaada mapema uelekezwe jinsi ya kufanya kuliko unavyoficha ficha na kujiona mjanja.

Inawezekana Wewe ndio umeanza muda si mrefu au una muda mrefu kuangala hizo movie au video za mapenzi au Video zinazoamsha Tamaa ndani yako lakini unasema mbona mimi naweza kijicontrol wala sipigi punyeto au hakunifanyi niwe na hamu za kufanya mapenzi na watu

Nu kweli unaweza usifike hatua ya Kufanya mapenzi na dada huyu au kaka huyu lakini hizo picha za uchafu au video za mapenzi unazoziangalia zitakuwa zinajengeka akilini mwako kiasi ya kwamba kila unapolala Unateswana mandoto ya Uasherati na kila siku unafanya uasherati au uzinzi na na majitu au watu fulani kwenye njozi zako.Ukiamka unajisikia raha kwamba umeshamaliza tamaa zako za mwili na unajiona salama kwakuwa hulala au hujatembea na dada au kaka yule, nikwambie wewe ni mzinzi au muasherati tu kama waasherati wengine

Ikiwa unataka kusaidika hakikisha acha kabisa kuangalia hizo video na au picha ambazo zinakupelekea kuchochea tamaa ndani yako

3)Kuruhusu Kusikiliza mazungumzo mabaya au kuwa na Marafiki wabaya
{1 WAKORINTHO 15:33}
[33]Be not deceived: Bad campany corrupt good characters.
Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

Hapa kuna maswala mawili yanazungumzwa ambayo yanaweza kuharibu tabia njema ya mtu hata kupelekea kuingia kwenye Tamaa mbaya ni
a)Mazungumzo mabaya
b) Marafiki wabaya

MAZUNGUMZO MABAYA

Tunaweza tukawa tupo safi kabisa kwenye utakatifu lakini pale tunaporuhusu Kukaa mahali ambapo kuna mazungumzo mabaya ua tunaporuhusu kupokea mazungumzo ya uchafu au ya uasherati

Kuna watu tabia zao ni kuhadithia tu habari za watu walioshindwa na kuwachafua watu kwa kueleza uchafu wao , utasikia anakutajia huyu kazini na huyu na yule katembea na yule.Tena anakutajia watu ambao ukiwasiliza huwezi kuamini na ulikuwa unawaamini sana hivyo mazungumzo yoyote ya kuelezana uchafu wa watu wanayofanya si tu yanaharibu tabia njema ya mtu bali yanachochea sana tamaa za mwili maana unaporuhusu mazungumzo ya kusikia habari za kushindwa au kuanguka kwa huyu au yule mara kwa mara inafika hatua unaona kumbe ni kawaida hayo kufanyika na inageuka kuwa roho kwako na itakufanya na wewe uchukulie kawaida

Lakini katika mazungumzo inaelezea pia mawasiliano! Moja ya mtego mkubwa unaoanza kuvuta hisia za mapenzi haraka ni mazungumzo katika mawasiliano kupitia Sms/ujumbe za kawaida either kwenye simu zetu au kwenye mitandao ya kijamii

Utakuta Kaka na dada wanawasiliana facebook au whatsap au Kwenye Sms za kawaida na wanaweza wakaanza vizuri kabisa na wala wanaweza wasiwe wanachat uchafu uchafu kwenye hayo mazungumzo yao, lakini hatua kwa hatua inafika hatua mmeshazoeana sana, na kupelekea huyu dada yuko huru kukuambia chochote bila shida na wewe vivyo hivyo. Mawasiliano haya yanapozidi na kuwa kawaida utaona tu hata kama ulikuwa hukuwai kumuwaza au kumfikilia kwamba utampenda lazima mawazo ya kuanza kumpenda yataanza kujengeka! Kama sio kwake basi kwako kutokana na hizo affection .

Hili swala nimeshalifanyia utafiti na nalifahamu vizuri hata kama upo vizuri vipi kiroho lazima mawasiliano au mazungumzo ya mara kwa mara na wadada lazima yatakuingiza katika mawazo au kuwa na hisia na huyo dada za kimapenzi.Maana moja ya kitu kinachochea upendo ni pale unapoona mtu anakujali , anakukumbuka, anakusalimia mara kwa mara, anawasiliana na wewe mara kwa mara. Hapo ndio mwanzo unaanza kuwaza au ndio mke Bwana kanieletea

Na Wengine wanaweza wakawa hawafahamiani kabisa wala hawajawai kuonana lakini kupitia hii mitandao utakuta watu wameshazoeana na hata wengine wameshakuwa wapenzi kwa njia za mitandao. Yaani wanatongozana humo humo, wanapanga mipango yao ya baadae humo humo inabaki kukutana tu. Ukiona sms zao utacheka yaani full kujiachia,

Utasikia huyu anamwambia "Hi Baby nimekumiss jamani" . Ebu nikiss basi kabla sijalala. Utasikia anakuita mme wangu au mke wangu ! Sijui hiyo ndoa wamefunga lini? Hawa ninaoeleza hivi ni watu ambao unakuta wametongozana tu humo humo mitandaoni. Wengi wanakuwa majasiri sana wa kuchat na kuongea hasa wakiwa wanatype mitandaoni yaani vidole vinaandika kama mashine ila wakikutana kwa mwanzo mwanzo wote madomo zege

Ndugu yangu inawezekana wewe ndio umeanza mawasiliano ya namna hii, nakusihi kwa Jina la Yesu Acha, maana utaenda mbali sana na mwisho wa siku si tu unachochea tamaa za mwili bali mwisho wa siku utajonyoosha na kupoteza mpango wa Mungu alioukusudia maisha mwako. Hata wewe ambaye umefika hatua hizo‼ Ebu acha mapema hizo tabia. Usione kwamba wewe ndio unajua kuchat, wewe ndio HB unajua kupendwa kuliko wote!! Ni shetani anakutega anataka akuzamishe kabisa kwenye hizo tabia ufike mbali (POINT OF NO RETURN) . ACHA ACHA ACHA. Aonywaye mara nyingi atavunjika shingo

MARAFIKI WABAYA

Moja ya maeneo ya msingi sana ambayo kama kijana na kweli umedhamiria kwenda mbinguni, ni katika uchaguzi wa marafiki. Ukishindwa kuchagua marafiki wazuri lazima tu utarudia katika dhambi iliyokuwa inakuzinga kwa upesi

{WAEBRANIA 12:1}
Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, NA DHAMBI ILE ITUZINGAYO KWA UPESI ; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

Ni Muhimu kufahamu hata baada ya kuokoka kuna dhambi ambazo zitakuwa zinatunyemelea kwa ukaribu na hasa Moja ya dhambi hizo ndio hizo zinazoitwa Dhambi zinazomzinga mtu kwa upesi ambazo ndio zile zilizokuwa zinatuvuta kwa haraka kabla ya kuokoka.Kila mtu anakumbuka kuna dhambi fulani fulani zilikuwa ndio zinamtumikisha sana kabla ya kuokoka

Sasa ninachokizungumza hapa ni juu yako ambaye unajua dhambi za Tamaa za mwili kama uasherati au uzinzi, Mawazo mabaya, Kupiga punyeto, Kupenda penda wadada n.k ndio zilikuwa ni dhambi zinazokuzinga kwa upesi kabla ya kuokoka, Hauna budi kuepeuka mazingira yote yanayoweza kukufanya urudie kule ulipokuwa.Kumbuka nilikueleza kuwa kuna mambo ukimpa ibilidi nafasi na kuyatengeneza wewe lazima tu utanashwa na mtego wa shetani

Sasa miongoni Mwa watu wanaohusika sana na kwa haraka Kuturudisha Nyuma hasa kurudia kufanya zile dhambi tulizokwisha kuziacha ni MARAFIKI WABAYA .Rafiki ni mtu ambaye ana nguvu sana ya kiushawishi na ni ambaye ni rahisi kumsikiliza na kufanya maana Wawili hawawezi kutembea pamoja wasipopatana AMOSI 3:3 . Ndio maana Baada ya kuokoka jambo la msingi sana ni kuvunja urafikk wa pete na kidole na Wale marafiki zetu ambao ndio walikuwa vichocheo vikubwa vya kutupeleka kwenye Kupenda penda kufanya uasherati, Kupenda kufanha starehe.

Baada ya Kuokoka Urafiki wote wa uboyfriend na Ugirlfriend wote unavunjia hata mawasiliano ni mwiko, maana ukiruhusu hilo lazima tu utanaswa na utarudia dhambi zako zile zile za Mwanzo ulizokuwa unafanya. Ikiwa umeshamwambia umeokoka, basi achana nae msiendeleze urafiki wala mawasiliano nae

Lakini tunatakiwa tutafute marafiki wenzetu wenye imani moja na sisi ambao si tu wanasema wameokoka bali ni moto ambao hawapendi dhambi wala mahusiano yoyote ya kimapenzi kabla ya ndoa. Ukiruhusu urafiki wa karibu na watu ambao stori zao na maneno yao ni mapenzi mapenzi na huyu ana girlfriend huyu na yule ana uboyfriend na yule, hapo lazima na wewe utanasa na utarudia hali yako ya Mwanzo ZABURI 119:63

{MITHALI 22:24-25}

Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi ;Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi Usije ukajifunza njia zake ;Na kujipatia nafsi yako mtego.

Ikiwa unajua huyu au yule ni rafiki yako hana anachokuongezea kuwa mbali na uchafu na tamaaa za mwili,bali ndiye anahusika kukufanya urudi kwenye uchafu uliouacha huyo usimpe nafasi usije ukajipatia mtego nafsi yako

Kama Biblia imesema Bad campany(Marafiki wabaya) destroy good character(huharibu tabia njema) basi usijifanye una busara kuliko biblia lazima tabia yako itaharibika ukifanya urafiki na watu ambao wanachochea urudi kwenye ile dhambi inayokuvuta mara ya kwanza.

Yapo maeneo mengi kama nilivyosema ila nimeona nitaje haya maeneo matatu makuu ambayo yatakupa mwanga wa kile ninachokimaanisha

Hivyo cha muhimu Inatupasa kujilinda sana na maeno yote ambayo yanaweza kutupatia mitego nafsi zetu hata kujikuta tukavutwa na Roho hizi za Uchafu na tamaa mbaya ambazo ibilisi amezimwaga nyakati hizi za mwisho. Biblia imesema itakuwa kama nyakati za sodoma na gomora au wakati wa Lutu hivyo utashangaa viwango vya ushetani vitaongezeka zaidi kadiri ile siku inavyokaribia.

Ni Muhimu Kukaa kwenye Neno la Mungu na Maombi kama tulivyoona hapo mwanzo ili kujilinda na kushindana na kila hali inayokuja kutukumbusha au kutufanya tuvutwe na tamaa hizi ,lakini zaidi sana kutoruhusu kutengeza mazingira ambayo yatatuingiza kuchochea tamaa hizi zililala .Nimeona nielezee haya kwa kwa leo ila usiache kufuatilia Masomo yanayohusiana na Hizi Tamaa mbaya ambayo bonyeza link hiyo utayapata mfulilizo wote kuanzia mwanzo hadi mwisho

Sehemu ya 1 - JINSI YA KUSHINDA TAMAA ZA UZINZI NA UASHERATI

KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USHAURI
Na: Shujaa Charles Richard Mwaisemba
0712-054498/ 0759-420202
stmwaisembac@gmail.com JINSI YA KUSHINDA TAMAA ZA MWILI (Sehemu ya Pili)

Reactions

Post a Comment

0 Comments