Historia, Maana, Lengo la Kitabu cha wimbo ulio bora

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

Wimbo wa Sulemani



Mwandishi: Sulemani aliandika Wimbo wa Sulemani, kwa mujibu wa msitari wa kwanza. Wimbo huu ni moja ya nyimbo 1,005 ambazo Sulemani aliandika (1 Wafalme 4:32). Anwani "Wimbo ulio Bora " ni sifa ya juu kabisa, kumaanisha huu ndio bora zaidi.

Tarehe ya kuandikwa: Sulemani huenda aliandika wimbo huu wakati wa mwanzo wa utawala wake. Hii huenda ikaweka tarehe ya utungaji karibu na 965 kk

Kusudi la Kuandika: Wimbo wa Sulemani ni shairi la hisia lililoandikwa kusifu wema/maadili ya mapenzi baina ya mume na mke wake. Shairi linatoa wazi ndoa kama mpango wa Mungu. Mwanamume na mwanamke waishi pamoja katika mazingira ya ndoa, wakipendana kiroho, kihisia, na kimwili.

Kitabu hiki kinapambana na sehemu mbili: Kujinyima raha na anasa (kukataa raha/anasa/starehe zote) na maisha ya anasa (ukimbiziaji tu wa raha/anasa/starehe). Ndoa iliyoelezwa katika Wimbo wa Sulemani ni mfano wa huduma, kujitolea, na furaha.

Mistari muhimu: Wimbo wa Sulemani 2: 7; 3: 5; 8: 4 - "Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini, msiyachochee mapenzi, wa kuyaamsha,hata yatakapoona vema yenyewe."

Wimbo wa Sulemani 5: 1 "- kaleni, rafiki zangu, kanyweni, naam, nyweni sana, wapendwa wangu. "

Wimbo wa Sulemani 8: 6-7 - "Nitie kama muhuri moyoni mwako, kama muhuri juu ya mkono wako; kwa maana upendo una nguvu kama mauti, na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, na miali yake ni miali ya Yahu. Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo mali yote ya nyumbani mwake, angedharauliwa kabisa. "

Muhtasari kwa kifupi: Utunzi wa shairi unachukua mtindo wa mazungumzo kati ya mume (mfalme) na mke wake (kutoka Ashuru). Tunaweza kugawanya kitabu katika sehemu tatu: uchumba (1: 1 - 3: 5); harusi (3: 6 - 5: 1); na ndoa komavu (5: 2 - 8:14).

Wimbo unaanza kabla ya harusi, kama bibi harusi anatamani kuwa na mchumba wake, na anatazamia kwa mpapaso wa mapenzi ya moyoni. Hata hivyo, yeye anashauri kuruhusu upendo kujiendeleza kiasili, kwa wakati wake mwenyewe. Mfalme anasifu urembo wa mke kutoka Ashuru, akishinda hofu yake ya jinsi anavyoonekana. Mke kutoka Ashuru anakuwa na ndoto ambapo anampoteza Sulemani na anamtafuta katika mji mzima. Kwa msaada wa walinzi wa mji, anampata mpenzi wake na kumkumbatia, akimchukua mahala pa usalama. Baada ya kuamka, anarudia amri zake za kutolazimisha upendo.

Katika usiku wa harusi, mume tena anasifu urembo wa mke wake, na katika lugha yenye mfano, mke anamkaribisha mume wake washiriki katika yote anayopaswa kutoa. Wanafanya mapenzi, na Mungu anabariki uhusiano wao.

Kama ndoa inavyokomaa, mume na mke wanapitia wakati mgumu, unaoashiriwa katika ndoto nyingine. Katika ndoto hii ya pili, Mke kutoka Ashuru anamkataa kwa dharau/anampuuza mumewe na anaondoka. Kwa kushindwa na hatia, anamtafuta katika mji; lakini wakati huu, badala ya walinzi kumsaidia wanampiga-ishara ya dhamiri yake ya uchungu. Mambo yanaishia kwa furaha wapenzi wanaporudiana na kupatanishwa.

Wimbo unapoisha, mume na mke wana ujasiri na usalama katika mapenzi yao, wanaimba kuhusu asili ya kudumu kwa mapenzi ya kweli, na wanatamani kuwa katika uwepo wa kila mmoja.

Ishara: Baadhi ya wakalimani wa Biblia huona katika Wimbo wa Sulemani uwakilishi halisi wa mfano wa Kristo na kanisa lake. Kristo anaonekana kama mfalme, wakati kanisa linawakilishwa na mke kutoka Ashuru. Wakati tunaamini kuwa kitabu kinapaswa kueleweka kawaida kama picha ya ndoa, kuna baadhi ya mambo ambayo yanaashiria Kanisa na uhusiano wake na mfalme wake, Bwana Yesu. Wimbo wa Sulemani 2: 4 unaelezea uzoefu wa kila muumini ambaye anatafutwa na kununuliwa na Bwana Yesu. Tuko katika mahali penye utajiri mkubwa wa kiroho na tumefunikwa na upendo wake. Mstari wa 16 wa sura ya 2 unasema: "mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake. Hulisha kundi lake penye nyinyoro "(NKJV). Hapa kuna picha si tu ya usalama wa muumini katika Kristo (Yohana 10: 28-29), bali ya mchungaji mwema ambaye anajua kondoo wake – waumini - na anautoa uhai wake kwa ajili yetu (Yohana 10:11). Kwa sababu yake, hatuchafuliwi tena na dhambi, tukiwa tayari "makovu" yetu yamekwisha kuondolewa kwa damu yake (Wimbo wa Sulemani 4: 7; Waefeso 5:27).

Vitendo Tekelezi: Dunia yetu imechanganyikiwa kuhusu ndoa. Kuenea kwa talaka na majaribio ya kisasa ya kutafsiri upya ndoa unasimama dhahiri kupingana na Wimbo wa Sulemani. Ndoa, anasema mshairi wa kibiblia, inapaswa kusherehekewa, kufurahiwa, na kuheshimiwa. Kitabu hiki kinatoa baadhi ya miongozo tendaji halisi ya kuimarisha ndoa zetu:

1) Mpe mpenzi wako makini anaohitaji. Chukua muda kwa kumjua kwa kweli mpenzi wako.

2) Kutia moyo na kusifu, si kukosoa, ni muhimu kwa uhusiano wenye mafanikio.

3) Jifurahie wenyewe. Panga matembezi fulani. Kuwa wabunifu, hata wacheshi, na kila mmoja wenu. Furahia kwa zawadi ya Mungu ya mapenzi ya ndoa.

4) Fanya chochote ambacho ni muhimu kumwahakikishia ahadi yako ya kujitolea kwa mpenzi wako. Weka upya nadhiri zenu, suluhisha matatizo na msichague talaka kama suluhu. Mungu anakusudia kwa ajili yenu wawili mwishi katika mapenzi salama na amani tele. 
Reactions

Post a Comment

0 Comments