Kitabu cha Mhubiri
Mwandishi: Kitabu cha Mhubiri hakimtambui mwandishi wake moja kwa moja. Kuna misitari michache sana ambayo inadokeza kwamba Sulemani aliandika kitabu hiki. Kuna baadhi ya vidokezo katika mandhari ambavyo vinaweza kupendekeza mtu tofauti aliandika hiki kitabu baada ya kifo cha Sulemani, pengine miaka mamia kadhaa baadaye. Bado, imani ya kawaida ni kwamba mwandishi kweli ni Sulemani.
Tarehe ya kuandikwa: Utawala wa Sulemani kama Mfalme wa Israeli ulidumu tangia takribani 970 BC hadi takribani 930 KK. Kuna uwezekano kuwa kitabu cha Mhubiri kiliandikwa kuelekea mwisho wa utawala wake, takriban 935 KK
Kusudi la Kuandika: Mhubiri ni kitabu cha mtazamo. Nakili ya "Mhubiri" (KJV), au "Mwalimu" (NIV) inaonyesha huzuni inayotokea kutokana na kutafuta furaha katika vitu vya ulimwenguni. Kitabu hiki huwapa Wakristo nafasi ya kuona dunia kupitia macho ya mtu ambaye, ingawa mwenye busara sana, anajaribu kutafuta maana katika vitu vya binadamu visivyodumu. Zaidi kila aina ya starehe za kidunia imetafitiwa na Mhubiri, na hakuna hata moja yazo inayompa maana hata kidogo.
Mwishoni, Mhubiri anakubali kwamba imani katika Mungu ndio tu njia pekee ya kupata maana binafsi. Anaamua kukubali ukweli kwamba maisha ni mafupi na hayana dhamana bila Mungu. Mhubiri anamshauri msomaji kuzingatia kwa Mungu wa milele badala ya starehe za muda mfupi.
Mistari muhimu: Mhubiri 1: 2, "Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili" (NKJV).
Mhubiri 1:18, "Yaani, katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni; Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko. "
Mhubiri 2:11, "Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua."
Mhubiri 12: 1, "Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.”
Mhubiri 12:13, "Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.”
Muhtasari kwa kifupi: Maneno mawili yamerudiwa rudiwa katika Mhubiri. Neno lililotafsiriwa kama "ubatili" katika KJV, na " bila maana" katika NIV yanaonekana mara nyingi, na yanatumiwa kusisitiza asili ya kutodumu kwa vitu vya kidunia. Mwishoni, hata mafanikio ya kuvutia zaidi ya binadamu yataachwa nyuma. Maneno "chini ya jua" yanaonekana mara 28, na yanarejelea kwa dunia yenye kufa. Wakati Mhubiri anarejelea "mambo yote chini ya jua," anazungumzia mambo ya kidunia,yasiyodumu, mambo ya kibinadamu.
Sura za kwanza saba za kitabu cha Mhubiri zinaelezea mambo yote ya kidunia "chini ya jua" ambayo Mhubiri anajaribu kutafuta ukamilifu kwayo. Anajaribu ugunduzi wa kisayansi (1: 10-11)., hekima na falsafa (1: 13-18 ), furaha/kicheko (2: 1), pombe (2: 3), usanifu (2: 4), mali (2: 7-8), na anasa (2: 8). Mhubiri aligeuza mawazo yake kuelekea falsafa mbalimbali kupata maana, kama vile uyakinifu (2: 19-20), na hata kanuni za maadili (ikiwa ni pamoja na sura 8-9). Alipata kuwa kila kitu hakikuwa na maana, njia ya mchepuko ya muda kwamba, bila Mungu, hakuwa na lengo au udumizo.
Sura 8-12 ya Mhubiri zinaelezea mapendekezo na maoni ya Mhubiri jinsi ipasavyo kuishi. Anaafikia hitimisho kwamba bila Mungu, hakuna ukweli au maana kwa maisha. Ameona maovu mengi na kutambua kwamba hata mafanikio bora zaidi ya mtu hayana thamani yoyote mwishowe. Hivyo anamshauri msomaji kukiri Mungu kutoka kwa ujana (12: 1) na kufuata mapenzi yake (12: 13-14).
Ishara: Kwa majivuno yote yaliyoelezwa katika Kitabu cha Mhubiri, jibu ni Kristo. Kulingana na Mhubiri 3:17, Mungu anahukumu wenye haki na waovu, na wenye haki ni wale tu walio katika Kristo (2 Wakorintho 5:21). Mungu ameweka hamu ya milele katika mioyo yetu (Mhubiri 3:11) na ametoa njia ya uzima wa milele kupitia kwa Kristo (Yohana 3:16). Tunakumbushwa kuwa kujitahidi kutafuta utajiri wa duniani si tu majivuno kwa sababu hautimilizi(Mhubiri 5:10), bali hata kama tunaweza kuupata, bila Kristo tutapoteza nyoyo zetu na kuna faida gani katika hilo? (Marko 8:36). Hatimaye, kila chukizo na majivuno yaliyoelezwa katika Mhubiri yana dawa/tiba yake katika Kristo, hekima ya Mungu na maana tu ya kweli itakayopatikana katika maisha.
Vitendo Tekelezi: Mahubiri yanampa mkristo nafasi ya kuelewa utupu na kukata tamaa ambao wale wasiomjua Mungu wanakabiliana nao. Wale ambao hawana imani ya wokovu katika Kristo wanakabiliwa na maisha ambayo hatimaye yataisha na kuwa potovu. Ikiwa hakuna wokovu, na hakuna Mungu, basi si tu kwamba hakuna uhakika wa maisha, bali pia hakuna kusudi au mwelekeo kuelekea kwake aidha. Neno "chini ya jua," mbali na Mungu, linakatiza tamaa, ni katili, siosawa/sio haki, fupi, na "halina maana kabisa." Lakini pamoja na Kristo, maisha ni kivuli cha utukufu utakaokuja katika mbingu ambayo itapatikana tu kupitia kwake .
0 Comments