Kitabu cha Mithali

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

Kitabu cha Mithali



Mwandishi: Mfalme Sulemani ndiye mwandishi mkuu wa Mithali. Jina lake linaonekana katika 1: 1, 10: 1, na 25: 1. Tunaweza pia kuchukulia kuwa Sulemani alikusanya mithali na kuchapisha kuliko yake mwenyewe, kwani Mhubiri 12: 9 inasema, "Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi. " Hakika, jina la Kiiberania ‘Mishle Shelomoh’ limetafsiriwa "Mithali za Sulemani."

Tarehe ya kuandikwa: Mithali za Sulemani ziliandikwa mnamo 900 kk. Wakati wa utawala wake kama mfalme, taifa la Israeli liliafikia mnara wa kiroho, kisiasa, kitamaduni, na kiuchumi. Vile ambavyo sifa za Israeli zilipanda sana, ndivyo za Mfalme Sulemani zilipanda. Vigogo wa kigeni kutoka sehemu mbalimbali za dunia walisafiri umbali mkubwa ili kusikia usemi wa hekima wa Mfalme (1 Wafalme 4:34).

Kusudi la Kuandika: Maarifa si kitu zaidi ya mkusanyiko wa ukweli halisi, bali hekima ni uwezo wa kuona watu, matukio, na hali kama vile Mungu anavyoyaona. Katika kitabu cha Mithali, Sulemani anaonyesha nia ya Mungu katika mambo makuu na ya ubora na kwa pamoja, kawaida, hali za kila siku, pia. Inaonekana kwamba hakuna mada ambayo Mfalme Sulemani hakuwa makini kwayo. Masuala yanayohusu mwenendo binafsi, mahusiano ya kijinzia, biashara, mali, upendo, tamaa, nidhamu, madeni, ulezi wa mtoto, tabia, pombe, siasa, kisasi, na ucha mungu ni miongoni mwa mada nyingi ambazo zimeshughulikiwa katika mkusanyiko huu murwa wa semi za hekima.

Mistari Muhimu: Methali 1: 5, "mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia."

Mithali 1: 7, "Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu."

Mithali 4: 5, "Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu"

Mithali 8: 13-14, "Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; kiburi na majivuno, na njia mbovu, na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi; mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu."

Muhtasari kwa kifupi: Kufupisha Kitabu cha Mithali ni vigumu kidogo, tofauti na vitabu vingine vingi vya maandiko matakatifu, hakuna mandhari maalum au mwanzo wa hadhiti unaopatikana katika kurasa zake, vivyo hivyo, hakuna wahusika wakuu katika kitabu. Ni hekima ambayo inatawala sana - hekima kubwa ya kubashiri inayopita historia yote, watu, na tamaduni. Hata kusoma kutimiza wajibu wa hii hazina tukufu kunaonyesha semi za maana sana za Mfalme Sulemani yanahusu leo hii kama yalivyohusu takribani miaka elfu tatu iliyopita.

Ishara: Mada ya hekima na umuhimu wake katika maisha yetu inapata utimilifu wake katika Kristo. Tunaendelea kuhimizwa katika Mithali tutafute hekima, tupate hekima, na tuelewe hekima. Mithali pia inatuambia-na inarudia- kwamba kumwogopa Bwana ndio mwanzo wa hekima (1: 7; 9:10). Hofu yetu kwa ghadhabu ya Bwana na haki ndio inatuelekeza kwa Kristo, ambaye ni mfano halisi wa hekima ya Mungu kama ilivyoonyeshwa katika mpango wake wa utukufu wa ukombozi kwa wanadamu. Katika Kristo, "ambaye ndani yake zimefichwa hazina zote za hekima na maarifa" (Wakolosai 2: 3), tunapata jibu letu kwa kutafuta hekima, dawa ya hofu yetu kwa Mungu, na "haki, utakatifu na ukombozi" ambalo tunahitaji sana (1 Wakorintho 1:30). Hekima ambayo inapatikana tu katika Kristo inapingana na upumbavu wa dunia ambao unatutia moyo kuwa wenye hekima katika macho yetu wenyewe. Lakini Mithali pia inatuambia kuwa njia ya ulimwengu si njia ya Mungu (Mithali 3: 7) na inaongoza tu kwa kifo (Mithali 14:12; 16:25).

Vitendo Tekelezi: Kuna utendaji usiokatalika unaopatikana katika kitabu hiki, kwa majibu ya busara na yenye maana kwa kila aina ya matatizo tata yanapatikana ndani ya sura zake thelathini na moja. Hakika, Mithali ndio kitabu kubwa zaidi cha "jinsi-ya" kilichowahi kuandikwa kamwe na wale ambao wana hisia nzuri ya kuchukua mafunzo ya Sulemani moyoni watatambua kwa haraka ucha Mungu, mafanikio, na ridhaa ni yao kwa kuuliza.

Ahadi inayokaririwa kitabu cha Mithali ni kwamba wale ambao watachagua hekima na kumfuata Mungu watabarikiwa kwa njia mbalimbali: kwa maisha marefu (9:11); mafanikio (2: 20-22); furaha (3: 13-18); na wema wa Mungu (12:21). Wale wanaomkataa, kwa upande mwingine, watateseka kwa aibu na mauti (3:35; 10:21). Kumkataa Mungu ni kuchagua upumbavu kuliko hekima na ni kujitenga sisi wenyewe kutoka kwa Mungu, Neno lake, hekima yake na baraka zake. 
Reactions

Post a Comment

0 Comments