HISTORIA YA WALUTHERI

MJUE MUNGU ILI UWE NA AMANI | IJUE BIBLIA

Walutheri

Jump to navigationJump to search
Lebo ya Luther: msalaba, moyo na waridi
Walutheri nchi kwa nchi mwaka 2013


Walutheri ni jina linalotumika kuwataja kwa jumla wafuasi wa Yesu Kristo wanaozingatia mafundisho yaliyotolewa na Martin Luther katika karne ya 16.

Uenezi

Madhehebu ya Kilutheri yalienea nje ya Ulaya Kaskazini kule ambako Wajerumani na Waskandinavia walihamia, kama vile Marekani.

Barani Afrika Walutheri wako hasa katika nchi zilizokuwa makoloni ya Ujerumani, kama vile Tanzania, Namibia na Kamerun, lakini pia Ethiopia.

Idadi yao ni kama milioni 75 na wanazidi kuongezeka barani Asia na Afrika, huku wakipungua sehemu nyingine.

Wafuasi wao walio wengi wengi wanaishi Ujerumani milioni 12.5, Marekani 7.1, Uswidi 6.5 million, Ethiopia na Tanzania kila moja milioni 5.8, Indonesia 5.6.

Kwa kuwatazama kama asilimia ya wakazi katika nchi mbalimbali Walutheri ni jumuiya kubwa kabisa ya kidini katika nchi zote za Skandinavia, Estonia, Latvia, Namibia na jimbo la North Dakota la Marekani.

Muundo, imani, liturujia

Muundo wao wa kanisa ni ama dayosisi/jimbo au kanisa la kitaifa.

Asilimia kubwa ya Walutheri wako pamoja katika Shirikisho la Kilutheri Duniani (Lutheran World Federation) lenye makao makuu mjini GenevaUswisi.

Msingi wao ni Biblia ya Kikristo yenye vitabu 66 tu.

Walutheri husisitiza mafundisho ya Katekisimu zilizotungwa na Martin Luther. Mafundisho yake yalipofanywa kuwa rasmi, katika Ujerumani makanisa ya Kilutheri yaliendeshwa kama idara za serikali za sehemu za Kilutheri chini ya uongozi wa wataalamu wa teolojia, lakini katika karne ya 20 kanisa na serikali vilitengana.

Kumbe hali hiyo inadumu mpaka leo katika nchi za Skandinavia (Sweden, Norway, Denmark n.k.) ambapo wafalme waliamua kugeuza Kanisa zima la nchi zao kuwa la Kiinjili-Kilutheri. Ila Sweden Walutheri waliendelea na cheo cha uaskofu na desturi nyingi za Kanisa la kale, wakifanana zaidi na Waanglikana wa Uingereza.

Walutheri wote wanaadhimisha sakramenti 2, yaani Ubatizo na Chakula cha Bwana.

Reactions

Post a Comment

0 Comments