NAMNA YA KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA (1)

NAMNA YA KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA (1)

*NA: MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SIKU YA KWANZA*
*TAR 19 OCTOBER 2016*
*LENGO LA SOMO: KUJIFUNZA TUPATE KUJUA NAMNA YA KUOMBA ILI HALI YA KIROHO YA ARDHI ILIYO KWAMISHA MAENDELEO YAKO IPATE KUONDOKA*;

 Tuangalie sababu kadhaa hapa;

1 *Sababu ya kwanza*


*Mwanzo 3:17-19*

Akamwambia Adamu,Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako ,ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza,  nikisema,Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
Michongoma na miiba itakuzalia , nawe utakula mboga za kondeni;  
Kwa  jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi ,ambayo katika hiyo ulitwaliwa ;kwamaana  u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Biblia inasema “Ardhi imelaaniwa kwa ajili yako “ … Neno laana maana yake…..kutokustawi, kutokufanikiwa, kutokufurahi,kutokufikia kiwango cha mafanikio Mungu alicho kikusudia  kwa ajili ya maisha  yako….Ni kinyume cha Baraka.
》》Kwa hiyo Mungu  anamwambia Adamu ….ukitaka kujua ni kitu gani umebeba baada ya kunikosea…..maana yake kuna laana iliyoko kwenye maisha yako …. Sasa na kwa sababu hiyo ardhi iliyoko chini yako imelaaniwa .
Kwa lugha nyingine unaweza ukakuta ardhi ni nzuri tu lakini wewe uliyebeba hiyo laana inayoelekeza wewe  uliyeko kwenye ardhi usifanikiwe ….unapokanyanga hiyo ardhi inavurugikiwa hali yake….. Biblia inasema pia .. ardhi itakuzalia mapooza na miiba  maana yake  inatusaidia kujua ya kwamba …..Mungu hakuumba michongoma na miiba mwanzoni , kwa uchungu utakula mazao yake siku zote ,maana yake kama kula kwa uchungu ni adhabu maana yake hatukupangiwa  kula kwa uchungu lakini baada ya dhambi ndio mambo yakabadilika ; Biblia inasema kwa jasho la uso wako utakula chakula: Maana yake; hazungumzii jasho hili unaloliona linateremka , hii ni body mechanism tu ya kawaida ambayo Mungu aliiumba kwa mwanadamu….
Lakini hii inamaanisha ….. *utashindwa kutumia akili yako vizuri ili kuiendeleza ardhi iliyopo chini yako;* …au *Hakutakuwepo mahusiano ya akili na kilichopo kwenye ardhi  na kwa sababu hiyo utatumia nguvu zaidi  kwenye ardhi kuliko akili*
Ardhi imepata shida kwa sababu ya laana iliyobebwa na mtu.

2 *Sababu ya pili*
》》Mwanzo 4:11-12
Basi sasa umelaaniwa  wewe katika ardhi , iliyofumbua kichwa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako
Utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake ; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikoa duniani.
Hi ni tofauti na ile sura ya tatu..surs ys tatu laana iko ndani ya Adamu sura ya nne laana ipo ndani ya Ardhi …maana yake kila atakaye kanyanga ardhi laana itatoka chini na kumfuata
Huwezi kutulia mahali,unajaribu kujenga hapa pana kataa unajaribu kukaa hapa panakataa lakini haujajua ya kwamba unapata shida  kwa sababu ya shida iliyopo kwenye ardhi…uharibifu uliotokea kwenye ardhi unakufanya  kutotulia …Biblia isinge semesha masuala haya ingekua shida sana
Kuna tofauti ya kuombea ardhi ( kuna laana iliyopo ndani ya ardhi na  na laana iliyopo kwa my anayetumia ardhi)

3 *Sababu ya tatu*
》》2 Nyakati 7:12-14
Bwana akamtokaea Sulemani usiku, akamwambia , nimesikis ulivyo omba na mahalia hapa nimejichagulia kuwa nyumba yangu  ya dhabihu .
Nikizifunga mbingu isiwe mvua , tena nikiamuru nzige kula nchi au nikiwapelekea watu wangu tauni;
Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenekesha na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya  basi nitasikia kutoka mbinguni nan a kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao
Nataka tuone neon na  *kuiponya nchi yao*
Nchi maana yake ardhi (land) sio nation ….kwa hiyo hapa haizungumzii juu ya uponyaji wa taifa inazungumzia uponya wa nchi( land)
nNchi ni mipaka yenye ardhi halali na taifa ni kundi la watu waliokubalia kuwa na mfumo wa uongozi wa kuwaunga pamoja
Ndio maaana kweny Biblia familia inaweza kuwa taifa ..na watu wengi sana wengi sana wanapotaka kuliombea taifa …
Haizungumzii  juu ya uponyaji wa watu bali uponyaji wa ardhi amabayo watu wanakaa
》》Neno ikiwa maana yake, kuna sehemu sentensi imeanzia …
Biblia inasema .. *” nikizifunga mbingu isiwe mvua“*  kama ukosekanaji wa mvua  katiaka eneo lenu unatokana na kufungwa kwa mbingu … maana yake mbinu inaweza na mawingu  lakini mvua isinyeshe
Biblia inasema tena … *” tena nikiamuru nzige kula nchi”*……maana yake wadudu waharibifu watakuja kuharibu kuharibu vitu vilivyopo kwenye ardhi
*”Tena nikiwapa watu wangu tauni”*…..tauni ni ugonjwa wa kuambukiza ambao ukienda kibiblia unahusiana na shida iliyopo kenye ardhi…Ndio usipojua vizuri utashindwa namna ya kuomba na inaweza ikakusumbua sana
Unaweza kuutumia huu mstari kuombea taifa ni sawa kabisa lakini uwe na uhakika kuna vitu havitatokea , hauta ona matokeo yake …wewew utakuwa una tafuta uponyaji wa watu lakini Mungu anaangalia uponyaji wa Ardhi, mnatazama vitu viwili tofauti….ni kama Mungu anasema umpokee kiwanja cha ndege cha Iringa wewe unaenda kumpokea Dar.
Mungu anapo weka mstari wa ahadi cheki mwiso wake. Itafsiri Biblia jinsi ilivyo, Cheki Mungu ameahidi nini lasivyo utapata shida sana .

4 *Sababu ya nne*
》》Yeremia 22:29-30
Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neon la Bwana
Bwana asema hivi, Andikeni habri za mtu huyu kwamba hana watoto , kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zote ; maana hapana mtu katika uzao wake akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi na kutawala tena katika Yuda.
Unaombaje wakati ardhi imepewa amri na agizo kwamba ; Hautafanikiwa wewe wala watoto wako.Huyu ni Mungu anazungumza nan chi (ardhi)……Maana yake ardhi au udongo unaweza kutunza kumbukumbu….inaweza kufuatilia kumbukumbu zilizopo ndani.
Wakati adhabu inatolewa kwa mtu huyu alikuwa bado hana watoto , kwa hiyo kumbukumbu kwenye ardhi ni kwamba  ni kwamba hana moto na kumbukumbu zina sema kwamba hata atakapopata watoto hata fanikiwa .

Adhabu ilitolewa kwa sababu gani; cheki ule mstari wa 21 …..huyu mtu alifanikiwa mwazoni lakini kutokana na kutotii sauti ya Mungu ; Mungu akasema its ok ngoja niondoe hayo mafanikioa  na ardhi inisaidie kuweka kumbukumbu kwa sababu huyu jamaa yupo duniani  atakanyanga ardhi tu na ardhi ishaandika hana motto na atakapoppata watoto hatawatafanikiwa maisha yao yote.
Fikiria wewe ni motto na umeingia kwenye adhabu ya baba au mama na unatafuta kufanikiwa na haufaninikiwi  sio kwamba akili huna no unazo lakini umezuiliwa kufanikiwa je unaombaje?
Haya ni masuala ambayo yapo  kawaida kabisa , wewe unaona wazazi wako walikuwa na  hali nzuri , wanaenda vizuri lakini ghafla hali yao ya mafanikio inaporomoka unajiuliza kuna shida gani imetokea … Biblia inasema wazi kabisa  …hawakutii sauti yangu wakati wa kufanikiwa kwao…Mwanzoni walifanikiwa kwa sababu walikuwa wananisikia sasa ninasema nao wakati wamefanikiwa hawanisikii  sas ngoja niwanyang’anye hicho kitu nilichowafanikisha ili wanisikie  … wewe ukafikiri ni adhabu yao tu  kumbe ni yakwako pia. Usipojua naman ya kuomba ni vigumu sana kutoka.

5 *Sababu ya tano*
_Mwanzo 28: 10-20
10 Yakobo akatoka  Beer-sheba , kwenda harani 11 Akafika mahali Fulani akalala huko usiku kucha , maana jua lilikuwa  limekuchwa ,akatwaa jiwe moja la mahali pale  akaliweka chini ya kichwa chake , akalala usingizi palapale 12 Akaota ndoto, na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni .Tena tazama malaika  wanapanda na kushuaka juu ya yake  13   Na tazama Bwana amesimama juu yake , akasema mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahim baba yako na Mungu wa Isaka , nch hii uilalayo ntakupa wewe na uzao wako
Nilitaka uone  lile Neno ..nchi hii ulalayo 
Nchi ni ardhi yenye mipaka halali ya umiliki,   sio kila mahali angeweza kulala  ila eneo lile lilikuwa na umiliki_ kamili wa Mungu ndio maana huyu ndugu alipo amka ule mstari wa 16 anasema ….” *Kweli Bwana yupo mahali hapa wala mimi sikujua* .
Ninachotaka uone , Ardhi unayolala  ,iwe ni nyumba uliyolala , au ni hotel,au kwenye basi au shambani halafu ghafla  ukaota ndoto , shukuru Mungu kwa sababu kakuonesha kinachoendelea katika ulimwengu wa Roho saa hiyo  saa ingine anaweza akakujulisha tafsiri yake baadae au asikujulishe kabisa … au unaamka unajikuta una hali tofauti na ile uliyokuwa nayo wakati ulipokuwa umelala
Alipo lala ardhi na roho ya umiliki ya mahali pale  ikaamua kumtembelea na kugusa maisha yake jumla , Mungu alijifunua kwake.
Na watu wengi sana wanapata shida au wanakwama kutegemeana na roho ya mahali wanapo lala. Ndio maana usipojua namna ya y kujikung’uta utapata shida sana na kitu ambacho unaweza kuwa umekutana nacho either kwenye hotel.. kikakutesa maisha yako jumla.
Nimeona wengine wamekuwa wakiteseka kutokana na mahali walipo lala wakiwa shuleni(bording)
Piawatumishi wengine  wakienda kwenye huduma  mahali wakatokewa na nuru wanafikiri ni Mungu na maisha yake ya huduma yana badilika completely na  na maana yake hakujua namna ya kuomba ,,,, alijiombea yeye akasahau ardhi ya mahali alipolala na hakuna mtu aliyemfundisha kuomba kwa stail hiyo.


  •  *Mfano* ., kuna mtu moja wakati tunafudisha somo hili kwa stail tofauti  yeye alikuwa yuko ulaya na sisi tupo Tanzania , akienda ulaya alikuwa halali na akija Tanzania ndio analala vizuri  kwa hiyo akitaka kupata usingizi mzuri anapanda ndege anakuja Tanzania  ana lala , akasikia tunafundsha na kuombea ardhi  ya mahali unapolala  akaomba jinsi tulivyo fundisha akiwa huko huko , Tangu siku hiyo akaanza kulala vizuri.

Angeenda hospitalini akaomba dawa kwamba Napata shida ya kupata usingizi  wangempa dawa yeye wasinge toa dawa kwa ardhi na atakunywa dawa na asinge lala , yeye angefikiri amelala kumbe wameichosha mishipa kwa dawa ,  dawa ikiisha na usingizi umeisha

6 *Sababu ya sita*
*2 Samweli 21:1*
Kulikuwa na njaa siku za daudi  muda wa miaka mitatu , mwaka hadi mwaka  naye Daudi akautafuta uso wa Bwana , Bwana akasema ni kwa ajili ya Saul, na nyumba yake yenye damu  kwa kuwa aliwaua hao wagibeoni.
Usishangae sana kuona hali ya njaa  ukasema hii haihusiani na hali ya kiroho ya ardhi.
Ukisoma ule mstari wa 14.. unaona Mungu anaiponya ardhi ;
Kwa hiyo Mungu alikuwa anaponya ili kumsaidia daudi kwenye kipindi chake ambapo kulikuwa na njaa kusiwe na njaa na kuwe na chakula …. Biblia inasema ….. alipata kibali ikaachiliwa Baraka, Baraka iliondolewa makusudi kabisa
Usishangae sana Daudi alikaa na upako lakini njaa ilikuwepo kwanini? Kwa sababu alishindwa kuunganisha shida ya njaa na tatizo la ardhi.  Hadi pale Mungu alipomwonesha .
Biblia inasema akatafuta uso wa Bwana kutaka kujua chanzo.

7 *Sababu ya saba*
*Ufunuo 12:12- 15*
Kwa hiyo shangilieni; enyi mbigu ,nanyi mkaao humo ole wan chi na bahari ! kwa maana Yule ameshuka kwenu kwenye ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana mda mchache tu
Na Yule joka alipoona ametupwa katika nchi alimwudhi mwanamke Yule aliyezaa  mtoto mwanaume
Mwanamke Yule akapewa mabawa mawili ya tai Yule mkubwa ili aruke aende zake nyikani , hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati mbali na nyoka huyo,
Nyoka akatoa katika kinywa chakenyuma ya huyo mwanamke maji kama moto amfanye kuchukuliwa na mto ule.

8 *Sababu ya nane*
*Yoeli  7:9-13*
Utaombaje ikiwa hali ya kiroho ya ardhi imesababisha sadaka zizuiliwe kutolewa kanisani.
Wachungaji wapo kanisani wao wanamwomba Mungu awasaidie  watu watoe sadaka sawasawa  Mungu ana sema hapana shida sio kutoa sadaka sawasawa sadaka zilikuz zinakuja ni mimi niliyezizuia  … badala ya kuombea wakristo ombea hali ya ardhi ya nyumbani kwao ..ikishapona ardhi swala la kutoa sadaka litakuwa rahisi sana

9 *Sababu ya tisa* 
*Kumbukumbu la torati 8 7-12*
Nilitaka uone lile neno kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake  ina mahusiano na Baraka za Mungu juu ya watu walioingizwa kwenye nchi  au kwenye mipaka halali ya umiliki
Ndio maana kati ya adhabu mojawapo inaifikia nchi ni miji kubomolewa au kukosa wakazi, kuwa ukiwa , kuwa mahame;…….laana aliyoilaani Yesu miji ya Bethsaida katiaka nchi ya Israeli tumepita kule ni magofu mpaka leo.

Biblia inazungumza Mungu  akirudia eneo anawapa na uwezo watu wliorudi kujenga pale kwa upya , wanajenga na wana kaa nadni yake . Na wale ambao Mungu aliwabbarikia na wakajenga halafu wakamkorofisha Mungu,  Biblia inasema watajenga na wasikae ndani.
*Pia kuna uhusiano gani  ulioppo kati ya ardhi na cheo….. kosa la kiti na kosa la mtu aliyekaa kwenye kiti  …. Kosa la kiti adhabu yake atapata kila mtu atakayekaa kwenye kiti… kwa hiyo kumfukuza kwa jinsi ya mwili kwa sababu amekosea haitutui tatizo la kiroho lililofanya akakose  kwa hiyo mtu mwingine atakayekuja atajikwaa palepale ….kwa sababu tatizo sio mtu ni kiti.*  Ndicho kilichompoza Daudi tataizo halikuwa kwake wala Sauli….tatizo ni maamuzi ya Sauli alipokuwa amekaa kwenye kiti. Sio kwamba daudi alirithi kiti alirithi na adhabu iliyokuwa kwenye kiti.
Kati ya jambo moja ambalo watu wamepata shida ni roho ya kukataliwa …ambayo ilimsumbua pia na Kaini……unakatataliwa na ngugu zako , unakataliwa na watoto wako , unakataliwa na mume au mke …. Kwa wachungaji unakataliwa na waumini bila maelezo. …. Unajiuliza ni kwa nini …. Ni ardhi iliyobeba roho ya kukataliwa…. Ndio maana kuna ardhi zinazo kataa wenyeji wasijenge kwao…unakuta wageni wana nyumba nzuri tu na sio kwamba wenyeji  hawana hela.
Baada yapo ni kufanya maombi ili kuondoa mapepo yote ya kukataliwa … wengine wanakataliwa na wachumba kumbe ardhi ilishasemeshwa asiolewe au asioe huyu….. na ardhi ikasema asioe huyu….
                  
*Kusoma Zaidi Mafundisho ya Mwl Mwakasege tembelea*
*Facebook*
https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/
Youtube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw
Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
website
www.mwakasege.org
*SEMINA IKO ITAKUWA LIVE YOUTUBE USTREM NA KWENYE* *www.mwakasege.org na www.kicheko.com*
  *Hallelelujh hallelujah Glory to GOD*
Endelea Kutufuatilia Jifunze Na Uelimike kwa muendelezo wa Mafundisho.

            Mw. Christopher Mwakasege

Reactions

Post a Comment

0 Comments