SOMO: SADAKA
UTOAJI KAMA MUALIKO WAKO BINAFSI KUTOKA KWA MUNGU
Kumbukumbu
12:10-11,13-14
13- Ujihadhali
usitoe sadaka kila mahali upaonapo/upapendapo (anywhere you please)
Ndugu hatuna amri/
ruhusa/machaguo (choice) ya kutoa sadaka popote tupendapo sisi
5 – Lakini mahali atakapopachagua BWANA, Mungu wenu (you are to seek the place the LORD, your God will choose….)
14- Bali katika mahali alipopachagua BWANA,
…..na kutenda yote nikuamruyo
-
Kutoa
kwa Imani ni kutoa kulingana na maelekezo amabyo umepewa na BWANA na sio ya
kwako ama upendavyo wewe kutoa sadaka.
-
Mungu
anaposema jihadhali maana yake kuna watu wengi wanapuuzia na kutoa sadaka kama
wapendavyo wao wenyewe ama viongozi wao.
-
Usitoe
kwa sababu watu wana shida , huo ni msaada na sio sadaka, Usitoe msaada ukaita
ni sadaka.
-
Sadaka
hutolewa kwa maelekezo toka (instructions) to kwa Mungu mwenyewe unayemtolea,
hata kwa waganga wa kienyeji hamtoi kile mpendacho bali kile waamurucho kutoa, Je
si zaidi sana kwa Mungu kutoa atuamurucho kutoa.
Je, Utajuaje kwamba hapo unapotolea sadaka ndipo BWANA
alipopachagua?
JIBU: Ni pale tu alipoamua kulikalisha jina lake (
alipoamua kuwepo sehemu hiyo); na sio mahali pa kuliitia jina lake.
Kumb: Jifunze kutofautisha mahali alipoliweka jina
lake na mahali pa kuliitia jina lake.
Mathayo 18:
20
Walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu,
nami nipo papo hapo katikati yao/ Pamoja nao
Key point | Wamekusanyika kwa jina langu –
alipochagua kuliweka jina lake
Sio popote
mkusanyikapo nyie jina lake linakuja, hapana mnapaswa kufuata mahali
alipoliweka jina lake, na ndio maana hema au hekalu halikujengwa popote ili
watu wawili watatu wakusanyike, walijenga alipochagua BWANA kukaa mahali hapo
uwepo wa Mungu unakuwepo.
-
Usitoe
Sadaka sehemu ambapo jina lake halipo / uwepo wake haupo
-
Biblia
haimuruhu mhubiri au mchungaji au askofu yeyote kuelekeza (Dikteti/Amuru) sehemu
ya kutolea sadaka.
-
Biblia
pia haimpi ruhusa mtoaji sadaka kuamua /kudikteti mahali pakutolea sadaka au
namna ya kuitoa sadaka hiyo.
-
Biblia
inasema usitoe mahali popote bali BWANA
atakapo pachagua na kuamua kulikalisha jina lake
-
Lolote
tulifanyalo tulifanye kwa jina lake, kumbuka kulitaja jina lake tu hakufanyi
pepo litoke maana kuna hata wanadamu wanaitwa majina wa kina yesu, Shetani (
Mapepo Jeshi) haogopi jina la Yesu anaogopa uwepo (presence ) wa mwenye jina
-
Wanafunzi
wa Yesu walipoulizwa kwa mamlaka/ amri ya nani ? na kwa jina la nani ? mna
fanya haya
Wakajibu;
Kwa jina la Yesu wa Nazareti,
mlie Msurubisha
-
Unapotoa
sadaka toa mahali ambapo jina lake limekaa hapo, maana yake palipo na uwepo
wake mwenye jina.
Mathayo 6:
26- Hazina ya mtu
ilipo, ndipo na moyo wake utakapo kuwa
Kwa kawaida tu mali zako zilipokaa ndipo
mawazo yako na akili yako yote ipawazapo na kupafikiria wakati wote.
-
MUNGU
anapotaka ulete sadaka yako anataka akutane na moyo wako,
-
Kwahio
basi, Unapotoa sadaka, tarajia kukutana na Mungu pale unapopeleka sadak
-
Mungu
akisema peleka sadaka kanisani atakupa na kanisa specific, sio uchague wewe
kanisa kwa sababu umeambiwa kupeleka kanisani.
-
Imani
huja kwa kusikia ila si mkila anayesikia huwa na Imani maana kama ni hivyo
ulimwengu mzima umesikia mahubiri toka kwa watu mbalimbali.
-
Imani
huja kwa kusikia Neno la Mungu, Ila Ili Neno liwe Imani lazima libadilike kuwa
personal instructions ( maelekezo binafsi ), Neno lisipokusukuma kuchukua hatua/matendo
(kufanya/kuacha) halijawa Imani hata usikie mara milioni.
-
Neno
la Mungu likikwambia nenda mahali Fulani kanitolee sadaka mahali hapo lazima
ukifika utakuta uwepo wake hapo.
Soma
Mwanzo 28: 10-22 Utakuta Habari ya Yakobo na uwepo wa Mungu alipolala mahli
pale Yakobo alifanya Nyumba ya Mungu.
Kama unauhakika (Imani)
ya kuwa Mungu ndiye aliyekuelekeza kutoa sadaka mahali alipokuelekeza kutoa
sadaka na ukafika hapo ukakuta uwepo wake haujajidhihirisha utafanya nini?
-
Kumbuka,
Mungu amekutuma uwende kukutana naye sio kutoa sadaka tu ( maana kama fedha-dhahabu
na mali zote ni zake, kama ni kondoo Wanyama wote wa kondeni/mbugani ni wake
akitaka anajitwalia)-mkumbuke Ibrahimu alibalikiwa kwa kukutana Mungu pa
kutolea sadaka.
- Usitolee sadaka na kuondoka kwa sababu amesema utoe sadaka mahali hapo, muombe Mungu ajidhihirishe mahali hapo huo ni uhuru wako kufanya hivyo
Mwanzo
22;1
kumbuka
Ibrahimu alipokuwa akiaandaa pa kutolea sadaka Mungu hakujidhihirisha mpaka
alipotaka kutoa sadaka. Kumbuka pia Mungu huchagua aina ya sadaka anayotaka
umtolee sio unayotaka wewe.
-
Watumishi
wa Mungu hawawezi kurudisha heshima ya Mungu, bali Mungu mwenyewe, hivyo hawawezi
kumtengenezea Mungu pa kutolea au kumchagulia aina ya sadaka ya kumtolea.
-
SOMA
Habari ya Gideoni kwenye kitabu cha waamuzi 6; 11-24
Gideoni
alimjengea Mungu Madhabahu mahali pale alipomuona malaika wa Bwana.
Ndio maana Mungu
anasema Beware/Jihadhalini
Kuna Nguvu za Mungu
zinakuwepo mahali halafu zinanyamaza, unatakiwa kuzi activate/ kuziamsha/kuzifanya
zifanye kazi, watu wengi huridhika wakikutana na wahubiri wakombewa matatizo
yao, wanasahau kuwa aliyewaita kwenda kumtolea sadaka sio muhubiri bali ni Mungu
kabla hawajakutana na Mungu wao wanarudi nyumbani wanaziacha sadaka zao, ndio
maana matatizo yao hayaishi kwani wahaubir ni saw ana mtu kuumwa malaria halafu
akanywa dawa za kutuliza maumivu . hamtibu magonjwa yenu badala yake mnapata
relief ( tumaini/faraja) utapona endelea kuamini mpendwa, wao sio Mungu
hakikisha umeuona uwepo wa Mungu ndio utoe sadaka.
Kutoka 25;
1-3,8
1-3- Wanitwalie
sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda…sadaka utakayo pokea
mikononi mwao ni hii…..
8- Nao
wanifaniyie patakatifu, nipate kukaa katikati yao
Unaona hapo juu
anasema ambayo moyo wako utapenda kutoa, lakini chini anasema sadaka utakayo
toa ni ipi, unaweza moyo wako ukapenda kutoa gari lakini Mungu akataka kuku,
kuwa makini mpendwa sadaka hutolewa na huagizwa kutolewa kwa malengo maalumu.
Swali ni je sadaka
tunayotoa kila siku za jumapili huwa ni ya nini/lengo lipi ?
Na ndo maana huwa tunatoa
chochote..tunatoa bila malengo/ makusudio…
-
Alipokuwa
anaagiza sadaka alikuwa anataka nini?
-
Ili
wamfanyie patakatifu, ili akae kati yao
-
Usitafute
motive yako( usisukumwe na hali yako/au mawazo yako) au ya muhubiri tafuta motive
ya Mungu kwenye kutoa sadaka, na motive ya Mungu ilikuwa kukaa kati yaw ana Israel
ili kukaa nao ilibidi watoe sadaka ili wajenge patakatifu.
-
Hema/Kanisa
sio sehemu ya ibada au ofisi ya Haruni/Mhubiri (ni Dwelling place-masikaniya Mungu na wanadamu-pa kukutana na Mungu
physical-katika mwili)
Kutoka 29;
10,42-46
10- ….mbele ya
hema ya kukutania
42- …..hema
ya kukutania mbele za BWANA, hapo nitakapokutana nanyi , ili ninene nawe hapo
43- ….nami nitakutana
na wana Israel mahali hapo , .. hema itafanywa takatifu kwa utukufu wangu
45- ..nami
nitakaa kati ya wana Israel, nami nitakuwa Mungu wao
-
Utukufu- ni uwepo wa Mungu kuonekana katika mwili mbele za
wanadamu (physical presence of God)-( Neno kufanyika mwili-Yohana 1; 1-10)
-
Ili
uwe na Imani lazima Neno lifanyike kuwa mwili; lazima uone tofauti katika
mwili-kungaa kwa sura ya Musa baada ya kukutana na Mungu
Hivyo mpendwa sadaka ni njia Mungu huitumia kukutana
watu wake na sadaka hufanya Mungu akae na watu wake hivyo hakikisha unapeleka
sadaka yako alipoliweka bwana jina lake na uwepo wake upo mahali hapo uwepo
ambao ukikutana nao utaona tofauti katika mwaili wako..kama aliuona Musa,
tusitoe sadaka kwa mazoea kwa sababu wachungaji wamesema tumtolee Mungu bali
Mungu mwenyewe akwambie umtolee..mengine yote tuyafanyayo sio sadaka bali ni
michango tu kama michango ya misiba, harusi na mingineyo..kama unatoa mali zako
kwa sababu umetaka wewe au umeagizwa na mchungaji hiyo sio sadaka..ni mchango
yu ..unpotoa pesa kuchangia ujenzi wa kanisa hiyo sio sadaka mpaka Mungu
mwenyewe amekwambia moyoni mwako..kama sivyo itakuwa ni mchango kama michango
mingine..
Unasema naongea nini unamiaka mingapi toka umekuwa
ukitoa sadaka kanisani ..ni sadaka ngapi umetoa bila kuona tofauti na ngapi
ulipotoa kuna kitu Mungu amekufanyia katika maisha yako.
Sadaka ambazo hazikuleta mabadiliko kwako hizo zote ni
michango sio sadaka, bali sadaka ni zile ambazo ulipotoa zilikukutanisha na
Mungu wako akafanya kitu kwenye Maisha yako..na macho yako yakawa shuhuda wa
hayo.
Kumbukumbu 12;13
Jihadahalini usitoe sadaka kila mahali upaonapo
Mungu akubariki san ana akupe kufuliwa macho ya rohoni
yakamuone, na masikio yako yakapate kusikia sauti yake ili upone.
By. Emmanuel M. Mhombwe +255763786083
0 Comments